Karibu green world-tanzania

Karibu kwenye kampuni ya Green world-Tanzania uanze safari ya mafanikio. Napenda kukupongeza kwa kuchagua ukurasa huu kwa sabababu umefanya uchaguzi sahihi utakaobadilisha maisha yako kifedha na kiafya. sasa chukua muda wako kupitia vipengele na huduma muhimu zitolewazo ndani ya kampuni ya green-world. hapa ndipo utafahamu malengo na makusudi yetu katika kukuwezesha ufikie ngazi za juu za mafaniko kwenye biashara ya mtandao huku ukitumia bidhaa zilizofanyiwa utafiti na kuthibitishwa na mamlaka za kimataifa kama ISO(international organization of standards).

1.Bidhaa za afya

kampuni ya green world iliamua kujikita kwenye utafiti na utengenezaji wa biadhaa afya ili kurudisha afya na kutibu magonjwa ambayo yameanza kuwa sugu na kushindikana.

Tunaamini kwamba binadamu wote tunapaswa kufurahia maisha pasipo kuumwa na kuteseka na magonjwa. Tumeumbiwa maisha yenye furaha na afya tele, swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza je tumefikaje hapa tulipo?, kwanini tunaumwa sana kuliko watu wa zamani?  Majibu yanaweza kuwa mengi lakini sababu kubwa ni lishe. Ndio ni lishe, lishe mbovu na uharibifu wa mazingia mazuri yanayotuzunguka imetufanya tuugue kila siku na kukosa furaha, ukianzia kwenye kemikali za kuua wadudu kwenye mimea, vyakula vilivyosindikwa, uchafuzi wa hewa na maji kutoka kwenye viwanda na tabia zingine hatarishi kama kutofanya mazoezi ni muunganiko wa hatari zinazopelekea tuumwe kila siku.

Sasa tujiulize tunaweza kuepuka moshi wa magari?, tunaweza kuepuka kula vyakula ambavyo vimelimwa bila kupigwa madawa?, tunaweza kuepuka kwa 100%, vyakula ambavyo havijapitia viwandani?, Jibu ni kwamba ni ngumu kuepuka kwa 100% hatari hizi zote maana ni sehemu ya maisha yetu kutokana na utandawazi na ugunduzi wa viwanda.

Tumaini letu lipo wapi?? Najua nawe pia unajiuliza tufanye nini sasa ili tuishi salama kama vihatarishi vyote hivi ni sehemu ya maisha yetu, tunafanya kazi viwandani, tunatumia maji yaliyotibiwa na kemikali, tunatumia vidonge, vipodozi na vyakula vyenye kemikali kwa wingi, muda mwingi tunautumia tukiwa tumekaa kwenye vitu, hatuna muda wa kufanya mazoezi sasa kwa mitindo hii ya maisha tunaweza kuepuka magonjwa kama kisukari, pumu, saratani, presha, upungufu wa nguvu za kiume, ugumba, kuvurugika kwa hedhi, na mengine mengi??

Habari njema ni kwamba bado kuna tumaini, ambalo litarudisha furaha na uwezo wa kuishi muda mrefu bila kuugua magonjwa ya lishe, magonjwa haya huwa napenda kuyaita magonjwa ya kisasa kutokana na kwamba yameshamiri sana kipindi hiki cha karne ya 21 baada ya ugunduzi wa viwanda. Tumaini letu ni kurudi zamani, ni kweli tunatakiwa kurudi na kutazama wapi tumekosea, babuzetu walikula nini na sisi tunakula nini, babu zetu waliishi vipi, walitumie dawa gani walipoumwa.

Hii ndio sababu yetu kuanzisha website hii ya Green world, KURUDISHA FURAHA ILIYOKWEPO MWANZO YA KUISHI PASIPO KUUMWA., ambapo tunalenga katika kutatua changamoto za magonjwa sugu kwa kutoa ushauri na huduma ya dawa asili zisizo na kemikali hatari kwa mwili na virutubisho ambavyo vitajenga mwili na kukidhi mahitaji yako ya madini na vitamini muhimu, virutubisho kwa ajili ya kutoa sumu mwilini na kuzawazisha homoni zako.unaweza kubonyeza hapa kufahamu kwa kina kuhusu bidhaa za green world.

2. Elimu ya biashara na jinsi ya kujiajiri ukiwa nyumbani(home based business)

Unaweza ukawa mmoja wa watu wanaojiuliza maswali haya, nina mtaji lakini sijui biashara gani ya kufanya?, sina mtaji je ni biashara gani ninayoweza kufanya kwa kuanza na mtaji mdogo sana?, nina hofu za kustaafu kwangu sina dira ni biashara gani nifungue ili nianze kutegeneza pesa kabla hata ya kustaafu, ni kampuni gani ya biashara ya mtandao itakufikisha kwenye mafanikio. maswali haya na mengine mengi utajibiwa kwenye website yetu. unaweza kuanza kwa kubonyeza hapa ili upate mafunzo ya awali juu ya biashara ya mtandao na kampuni ya green world. hapa chini nimekuwekea kwa ufupi faida tano utakazopata baada ya kujiunga na kampuni ya green world-Tanzania

FAIDA/NJIA 5 UNAZOWEZA KUTENGENEZA PESA UKIWA NA NETWORK MARKETING UKIINGIA UBIA NA KAMPUNI YA GREEN WORLD
  1. Faida ya mauzo ya rejareja kwa wateja wako, ambapo ni 15% ya bei unayouziwa dukani ikimaanisha kwamba unauziwa kwa punguzo la 15%
  2. Indirect Bonus, ambapo ni bonus unayopewa kutokana na mauzo yako mwenyewe
  3. Indirect bonus hii ni bonus ambayo unapewa kutokana na mauzo ya team yako ya biashara, nikisema team namaanisha kwamba unapoanza biashara na ukajifunza mbinu za kufanya biashara basi ndipo unavoweza kufanya duplication yaani kuwafundisha na wengine vile ambavyo wewe unafanya na ndipo utakapokuza kipato chako.
  4. Zawadi maalumu, hizi hutolewa kwa msambazaji mwenye kiu na mwenye kasi ya ufanyaji biashara, hata wewe unaweza kuipata, utafahamu unaipataje kwenye mafundisho ya baada ya kujiunga na biashara. Zawadi hizi ni kama magari, safari za kwenda nje, pamoja na nyumba.
  5. Faida ingine ni kwamba utapata mafunzo ya kufanya biashara bure kabisa kutoka kwa kiongozi wako aliyekutangulia, hapa ndipo utagundua kuwa network marketing ni darsa kubwa sana ambalo inahitaji kufungua ubongo na kufanyia kazi unachojifunza.
  6. Mwisho kabisa bidhaa zina ubora wa hali ya juu, hivo utaweza kutatua matatizo ya kiafya yanayoikumba familia yako, jamii inayokuzunguka na pia kutatua kero mbalimbali za wakulima. Hii itakuongezea thamani na umuhimu wako kwa jamii.

3. Shuhuda za mafanikio ndani ya kampuni ya Green world.

katika kuwaleta karibu wasomaji wa ukurasa wetu na kujenga uaminifu tumeweka hapa shuhuda za wanachana mbalimbali waliojiunga na Green world kwa jinsi walivyofikia mafanikio makubwa ya kifedha kwa kuwekeza tu muda. utapa ushuhuda pia kutoka kwa wagonjwa mbalimbali waliotumia dawa za green world na kupona kabisa, baadhi ya wagonjwa hawa walisumbuliwa na uvimbe kwenye kizazi(fibroids), kisukari, vidonda vya tumbo, kifafa, saratani, uzito mkubwa na kitambi na magonjwa mengine mengi. utasoma pia kufahamu shuhuda wa wakulima waliofanikiwa zaidi baada ya kutumia mbolea yetu ya asili (Green world organic fertilizer). Najua nawe utakuwa na hamu ya kuwa miongoni mwa wanachana wa Green world waliofanikiwa sana aidha katika biashara, kilimo au kiafya. Nirahisi sana kuungana nasi bonyeza tu hapa.

4.Bidhaa ya mbolea asili na kilimo chenye Tiba

mbolea ya green world
mbolea asili

Mbolea hii huhifadhiwa katika ujazo wa lita moja,ni mbolea isiyo na kemikali iliyotengenezwa na viumbe hai yani wanyama na mimea. Mbolea hii imetengenezwa baada ya utafiti wa kina kufanyika nchini Marekani. Kwakuwa imezingatia mahitaji yote ya mimea ikiwa ni pamoja na virutubisho vyote vinavyohitajika kwa wingi katika mmea (macro nutrients) mbolea hii ina madini ya Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Calcium, Magnesium na Sulpher.

 Pia mbolea yetu ya maji ina(micro nutrients) yaani madini au virutubishi vyote vinavyohitajika kwa kiwango kidogo katika mmea vikiwa ni Zinc,Ferrous,Copper, Boron,Manganese, Silicon,Molybdenum,Sodium, Cobalt na Chlorine.

 

Kwakuwa Amino acids ni muhimu katika ukuaji wa mmea, mbolea hii imesheheni aina zote nane za amino acids.Amino acids huusaidia mmea kukua haraka,kuwa na ujazo mkubwa,huusaidia mmea kupambana na magonjwa na nivigumu kuathiriwa na magonjwa mbalimbali.

Karibu nawe ufurahie uzuri wa mbolea yetu uwe mmoja wa mashuhuda. 

 

.