Biashara ya mtandao na green-world

Kabla hujajiunga na kampuni yetu ya green world unatakiwa kujifunza haya. Tafadhali usichoke kusoma maana umebakiza hatua chache kuanza safari ya mafanikio.

Fahamu kwa kina nini maana ya biashara ya mtandao au network marketing ambapo ndio mfumo unaotumiwa na kampuni yetu katika kuhudumia wanachama wake kifedha na bidhaa pia.

Network marketing au biashara ya mtandao ni nini?

Biashara ya mtandao ni mfumo ambao ulianzishwa uko ulaya kwa lengo la kuweza kuondoa tatizo la ajira na kuweza kurahisisha usambazaji wa bidhaa. Katika mfumo huu kunakuwa na muunganiko wa watu watatu yaani -kiwanda -msambazaji au mwanachama ambaye ndio wewe utakayejiunga na biashara na  mtumiaji ama mteja. Hapa ndipo msambazaji anapoingia ubia na kampuni aipendayo kufanya nayo biashara ili aweze kujitengenezea kipato. Katika mfumo huu msambazaji anapo nunua bidhaa kutoka kiwandani anamfikishia mtumiaji moja kwa moja. Mfumo huu mara nyingi unamnufaisha msambazaji kwakuwa zile gharama ambazo zinge gawanwa na wale wasambazaji pale katikati zote huzichukua yeye. Najua ni vigumu kuelewa kwa haraka lakini nakuhakikishia ukishaanza biashara ntakupa mafunzo kila siku mpaka uwe nguli ukabobea kwenye biashara.

ili uanze biashara hii ya network marketing lazma uingine ubia na kampuni, kisha baada ya hapo utakuwa ni msambazaji halali wa bidhaa za kampuni husika popote kwenye tawi la kampuni, manake utafanya manunuzi kwenye tawi tawi la kampuni na kisha utaweza kuuza kwa wateja wote popote na ukafaidika.na pia unaweza kufungua duka lako mahali popote Tanzania ukawekeza pesa yako na ukavuna pesa. Najua unatamani kufahamu zaidi kuhusu faida za network marketing sasa ebu endelea kujua utamu wake kabla hujajiunga nasi

FAIDA 6 ZA BIASHARA YA MTANDAO

  1. MTAJI MDOGO WA KUANZIA

Unaweza kuanza biashara ya mtandao kwa mtaji mdogo sana au kwenye kampuni nyingine bila kuwa na mtaji kabisa. Hakuna tofauti kati ya yule aliyenza na mtaji mdogo na yule aliyeanza na mtaji mkubwa, fursa zenu za kufika mnakotaka zinafanana na kubwa kuliko fursa utakayopata kwenye mifumo mingine ya biashara. Pamoja na kuwa pengine utaanza biashara yako bila mtaji wo wote, utahitaji kiasi fulani kidogo sana cha pesa kwa ajili ya uendeshaji wa biashara yako ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa, mawasiliano, usafiri, matangazo n.k.

Nchini Tanzania, kuna tuna ushuhuda dada ambaye alianza biashara kwa kutoa kiingilio cha Tshs  35,000/= kwenye (kampuni inayohusu afya ya binadamu), akaanza kwa kupeleka wagonjwa kupata tiba kwenye kampuni hiyo na kukua taratibu hadi kufikia kupata bonasi nzuri kila mwezi na kupewa tuzo ya gari lenye thamani ya milioni 18 katika kipindi cha mwaka mmoja tu – hakuwa na mtaji zaidi ya pesa ya kiingilio. Picha yake ndo hii ya hapa chini.

  1. MAFUNZO BURE JINSI YA KUENDESHA BIASHARA YAKO

Kila mwanachama anayejiunga na biashara hizi hupewa mafunzo ya kutosha. Mafunzo hayo utayapata kutoka kwenye kampuni au kutoka kwa mtu wa juu yako (aliyekusajili). Kampuni nyingine hutoa mafunzo ya aina mbali mbali kwa wanachama wao, hutoa mafunzo darasani, CD, DVD, vipeperushi na hata vijitabu vya kujisomea. Kwahiyo huhitaji kuwa na elimu kubwa ya mauzo au uzoefu wa kuuza bidhaa haya yote tutakufundisha pindi tu utakapojiunga na biashara

  1. UHURU WA KIFEDHA NA MUDA

Hivi ulishwahi kujiuliza ni bishara gani unaweza kuifanya ukiwa umelala chumbani kwako bila kwenda eneo la biashara? Au bila kufungua banda na kukodi ofisi?, najua unatamani kufanya baishara kwa kujisimamia mwenyewe huku ukiwa umekaa nyumbani kwako unafurahia maisha, sasa biashara ya mtandao itakupa yote haya, manake hakuna boss atakulazimisha kufanya kazi ni wewe mwenyewe utaamua siku za kufanya kazi. Unaeweza kutenga siku 3 tu ndani ya week na ukapiga pesa ndefu.

  1. UNAFANYA BIASHARA POPOTE DUNIANI KWENYE MATAWI YA KAMPUNI
    Biashara ya mtandao inakuruhusu kutumia bidhaa na kuuza mahali popote ambapo kuna tawi la kampuni husika, mfano kampuni yetu ya green world ina matawi Kenya, Uganda, Zambia, Africa kusini, Morroco, Zimbabwe, Urusi, Marekani, Tanzania, Canada, China, Indonesia  na nyingine nyingi, na kote huku unaruhusiwa kufanya biashara kwa kutumi kadi moja ya uanachana ambayo utapewa wakati unajiunga.
  2. BIDHAA ZA KIPEKEE AMBAZO HAZIPATIKANI MAHALI PENGINE POPOTE

Bidhaa zinazpatikana kwenye biashara ya mtandao ni bora na adimu sana, huwezi kuzikuta madukani, hii itakufanya wewe msambazaji kuwa mfalme maana utatengeneza orodha ya wateja wako wa kila siku, kila watakapotaka bidhaa yako inabidi wakutafute tena na tena na ndivyo utakavotengeneza bomba la pesa kuelekea mfukoni mwako.

  1. MALIPO YASIYOKUWA NA UKOMO (PESA ISIYOKAUKA) 

Kampuni za mtandao zinawapa fursa wanachama wao kupata malipo endelevu kwa kazi walizozifanya mara moja. Karibu kila mmoja wa watu wanaojiunga na biashara hizi huwa amevutiwa na aina hii ya malipo naamini hata wewe mpenzi msomaji wa makala yangu utafurahia jambo ili. Wewe kama mwanachama unamsajili mwanachama mara mmoja tu na mtu huyu akiendelea kununua bidhaa na kujenga timu inayofanya kazi vizuri, wewe utaendelea kulipwa tena na tena bila ushiriki wako wa moja kwa moja. Ndio maana nikasema hakuna biashara tamu kama hii, unatumia bidhaa huku unalipwa, unauza unapata pesa ya rejareja, bado kuna bonus za kila mwisho wa mwezi. Upewe nini sasa zaidi ya fursa hii.

NAKUKARIBISHA KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO

Sasa nakuruhusu tumia dakika tano kujitafakari, kama uko smart unaweza kutumia dakika moja tu maana najua hutasita sana kwa jinsi fursa hii ilivyo tamu. Baada ya kujifakari na kuridhika kwamba unataka kuanza biashara hii basi bonyeza maandishi ya blue hapa chini ili tuwasiliane kwa whatsapp uweze kulipia gharama ya kujiunga sh 35,000/= uanze biashara